Tuesday 17 January 2012

Jadi nilipokupenda,
wakti lolote ningetenda,
ahadi ulipanda,
nkatarajia kuvuna,
hisia na huba,
farha si haba,
kumbe haba na haba,
haujazi kibaba bin riba, loh!

Longo longo,
jicho la moyo nalo chongo, 
sikujua ni hongo, 
penzi ulonipa, 
heri ngetia usongo,
nsipumbazwe na udongo, 
umenifunza hata kwa matongo, 
samaki humjua papa!!

Dalili ulinipa,
ila macho nilifumba,
ulinifunga kwa kamba,
nami maskio nkatia pamba,
kama damu kwa mshipa,
nilikuthamini mahabuba,
sikujua wetu usuhuba,
ni mazigazi ya jangwa, loh!

Longo longo,
jicho la moyo nalo chongo, 
sikujua ni hongo, 
penzi ulonipa, 
heri ngetia usongo, 
nsipumbazwe na udongo, 
umenifunza hata kwa matongo, 
samaki humjua papa!

Ulinihadaa, nami nilikaa,
kijipa tumaini, ukanikeketa maini,
ulinikalfisha, ila mda wako umekwisha,
mbio za sakafuni, huishia ukingoni, 

Kibali

No comments:

Post a Comment