Saturday, 13 July 2013

Fahamu Fika

Sijui nikwambieje, moyo wangu watetema, 
hofu imenitanda mawazo yarandaranda, 
sidhani niko sawa
sijui nikwelezeje, bila wewe sina usalama naungama, 
pete kawaida huvikwa chanda walakin ni bayana tuko njia panda, 
pasi na wewe napagawa. 

Ila wanisusia, 
manake ushakuwa mchezo wa shere, 
yaogee maji ukishayafulia, 
keti utue mwaserere, 
kisha kama huoni gere, 
kunihadaa kuniacha nikiumia, 
haina kwere, 
mwafulani uchungu nishauzoea. 

Fahamu fika katika harakati za maisha, ah ah, 
ya dunia kawaida huisha ah ah, 
fahamu fika katika harakati za maisha ah ah, 
huba hufifia kisha. 
Naam najua, naam najua, 
naam najua, naam najua.

No comments:

Post a Comment