Saturday, 26 May 2012

Usodai


Kila safari ina mwisho,
Hata upawe ngapi vitisho,
Ufuoni hutoki bila kivukisho,
Tia maanani hamasisho,
Si kosa kumbeleza
Ila ukiamua wewe kunipeza,
Ni kibarua ushateleza,
Nami sasa nakueleza.

Sirai na sijidai,
Wala sina wakti wa kukanusha yako madai,
Moyo ukikinai,
Kinacho salia ni usodai'

Mengi yamesemwa  
Ila  mnazi sharti kugemwa,
Mate kwangu yametemwa,
Kisha washtushwa na zangu memwa (memoir),
Nimefunzwa na dunia,
Hatimaye ni vyema kughairi nia,
Swahiba wali kwa sinia,
Jua kwangu ukaidi hutonimiminia.

Sirai na sijidai,
Wala sina wakti wa kukanusha yako madai,
Moyo ukikinai,
Kinacho salia ni usodai

Uvumilivu huisha, wazuri hujatisha,
Kwako tena sitobisha, ndio hali ya maisha,
Subra imekwisha, ishu zetu nimesitisha,
Nlikudhamini ukanidhalilisha, ila shakuvua taji nlokuvisha.


PS:
Usodai (ukaidi) means arrogance, or pride based on context. While this piece uses a love relationship gone sour as its premise, every shade of skewed relationships applies. "When love (patience etc runs out and I can't stand your bulls**t anymore), arrogance takes over." No need to esteem them that treat you with disdain.

No comments:

Post a Comment