Moyo wangu umetanda, hisia zenye uzani,
Na mawazo yanikanda, yanibinya akilini,
Nuru ipo ila kuona sioni,
Godoro kichapo wala silali asilani,
Hapa nlipo niko taabani,
Hofu ipo, tadidimisha afueni,
Kila kukicha nawaza mustakabali,
Maswali yamechacha, najihoji tawaje jabali
Natamauka, natamauka
Chemichemi lakauka,
Ndoto zangu zanyauka,
Natamauka,
Natamauka,
Sitaki tena rauka,
Najihisi napauka
Nakaribia mauka
Sitosheki na uhalisia,
Manake nimekisia,
Kuwa wahed tangia,
Mistwari nianze jitungia,
Napambana na hizi hisia,
Takriban miaka tisia,
Mipango kemkem mejipangia,
Ila kasri Abadan katan sijaliingia
Natamauka, natamauka
Chemichemi lakauka,
Ndoto zangu zanyauka,
Natamauka,
Natamauka,
Sitaki tena rauka,
Najihisi napauka
Nakaribia mauka
Nlivo tamani himaya,
Nkaanza tunga riwaya,
Maisha kayapa hidaya,
Ufanisi uwe wangu muhibati bila haya,
Ilmuradi kujiepushia mashakaya,
Sasa hayo yote hekaya,
Meyeyushiwa deraya,
Mejaziwa maya,
Kila nkilala nagwaya,
Kama mtoto anaehitai yaya,
Gizani mekuwa kaya,
Mejawa na huzuni kayaya.
Napauka,
natamauka
nanyauka
nakaribia mauka.
Kibali
Mauko means death in old Swahili, and through poetic license decided to change that to Mauka denoting death of self. Shukran